Kikosi cha wapiganaji cha Abbasi kimefanya msako katika eneo lenye ukubwa wa kilometa (1750) kwenye opresheni inayo endelea ya “Makamanda wa Iraq”.

Maoni katika picha
Wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) Liwaau/26 Hashdi Shaábi katika opresheni ya (Makamanda wa Iraq) hatua ya kwanza, wamekamilisha msako katika eleo lenye ukubwa wa kilometa (1750) za jangwani na wanaendelea kutimiza jukumu walilopewa.

Kiongozi wa opresheni hiyo Sayyid Haidari Mussawi ameviambia vyombo vya habari kua: “Kikosi cha wapiganaji pamoja na Liwaau/16 ya wanajeshi wa muungano wanao shiriki kwenye opresheni hiyo, wameanzia Nakhibu kuelekea Baji-Bajibahah (km 70) na ndani ya jangwa (km 25)”.

Akabainisha kua: “Lengo la opresheni hii ni kuimarisha usalama katika jangwa na kuwasaka magaidi pamoja na wahalifu wengine”.

Tambua kua wapiganaji wa kikosi cha Abbasi walianza kazi hiyo Alfajiri ya jana katika mji wa Nakhibu, kwa kushirikiana na viongozi wa kikosi cha muungano na kile cha Furatu-Ausat, kusafisha mabaki ya magaidi wa Daesh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: