Zaidi ya watumishi 40 katika ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya mahusiano, imepokea jopo la watumishi zidi ya 40 kutoka idara ya malezi katika mji wa Baabil (Wilaya ya Kuful).

Ugeni huo ni sehemu ya ratiba maalum ya kupokea wageni kutoka sekta ya elimu na malezi kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel unao simamiwa na idara hiyo, unaolenga kuongeza hazina ya maarifa na kuwaonyesha miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya.

Ratiba ya ziara hiyo itaendelea kwa muda wa siku nne ikipambwa na mihadhara ya kifiqihi, kimaendeleo na mapumziko.

Pia kuna ziara ya pamoja katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) sambamba na kutambulisha miradi ya Ataba watakayo tembelea.

Kumbuka kua ratiba ya kupokea wageni inasimamiwa na idara ya uhusiano wa vyuo katika kitengo cha uhusiano chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea siku zote za mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: