Kumtumikia zaairu ni kauli ya kwanza katika vitengo vya Ataba tukufu kikiwemo kitengo cha utumishi

Maoni katika picha
Juhudi kubwa na huduma mbalimbali zinatolewa na idara pamoja na vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwemo idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi, kwa ajili ya kuandaa sehemu na mazingira ya kufanya ibada kwa wanaokuja kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuwapa mahitaji yote muhimu, hasa katika siku zinazokua na mazuwaru wengi.

Ustadhi Faakhir Zaair Abuud kiongozi wa idara ya usafi ameongea na mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Miongoni mwa kazi kubwa zinazo fanywa na idara yetu ni kusafisha jengo takatifu pamoja na maeneo yanayo lizunguka na sardabu, sambamba na kutandika mazulia na kusimamia usafi wakati wote ili kupafanya kua sehemu muwafaka kwa kufanya ibada, hupanga vikundi vya watumishi vinavyo fanya kazi ya usafi muda wote”.

Akaongeza kua: “Tuna kazi nyingi tunazo wafanyia mazuwaru, kama vile kuandaa sehemu za kutupia taka na kuondoa taka kila wakati, kwa kutumia mikokoteni maalum, pamoja na kuimarisha usafi katika eneo linalo zunguka haram tukufu, pamoja na kwenye vibaraza vya nyumba kuanzia kituo cha Alqamar hadi barabara ya Alqami, sambamba na kazi hiyo watumishi wetu hubeba wazee na watu wenye ulemavu kutoka Atabatu Abbasiyya hadi Atabatu Husseiniyya au kuwapeleka katika hoteli wanakoishi, pamoja na kuwapokea mazuwaru watukufu ndani ya sardabu, na kuwapa kila wanacho hitaji sambamba na kuwatengenezea mazingira mazuri yanayo wawezesha kufanya ibada kwa amani na utulivu.

Tambua kua Atabatu Abbasiyya hutoa huduma mbalimbali kwa watu wanaokuja kufanya ziara katika Ataba za Karbala, kwa ajili ya kuwawezesha kufanya ibada kwa amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: