Atabatu Abbasiyya imepambwa na furaha za kumbukumbu ya kuzaliwa mtoto wa Mtume (a.s).

Maoni katika picha
Kufuatia siku ya kukumbuka mazazi ya mbora wa wanawake wa ulimwenguni Fatuma Zaharaa (a.s), malalo ya mpenzi wake Abulfadhil Abbasi (a.s) imejaa furaha katika kuipokea siku ya kesho Jumamosi (20 Jamadal-Aakhar).

Mapambo na mauwa yamewekwa kwenye milango ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kila kona ya haram, jambo linalofanya mazuwaru wahisi furaha na amani, kuta za haram zimepambwa kwa vitambaa vilivyo andikwa ujumbe unaohusu tukio hilo adhim, pamoja na taa za rangi, bila kusahau mauwa ambayo yameipendezesha haram takatifu, mapambo yamewekwa hadi nje na katika uwanja wa katikati ya haram mbili hadi kwenye malalo ya bwana wa vijana wa peponi Abu Abdillahi Hussein (a.s).

Kuna ratiba maalum iliyoandaliwa na Atabatu Abbasiyya ya kuadhimisha mazazi haya yenye vipengele vifuatavyo:

  • - Kufanya hafla ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zitakazo ratibiwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, alasiri ya Ijumaa.
  • - Kuandaa hafla ya wajukuu wa Zaharaa (a.s) wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya usiku wa leo –siku ya mazazi matukufu- itakua na muhadhara pamoja na mashairi.
  • - Harakati za wanawake zitakazo ratibiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya na kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s).
  • - Kuandaa sehemu ya mazuwaru katika sardabu kwa ajili ya kusherehekea tukio hili.

Kutakua na harakati zingine ndani na nje ya Ataba zote zinalenga kuadhimisha tukio hili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: