Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chakamilisha hatua ya pili ya opresheni ya (Taifa langu Iraq).

Maoni katika picha
Chini ya mkakati madhubuti na ari kubwa, kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kimekamilisha hatua ya pili ya opresheni ya kijeshi iitwayo (Taifa langu Iraq) iliyo anza alfajiri ya jana siku ya Jumatano katika mji wa Nakhibu kuelekea jangwani.

Msemaji wa kikosi amesema kua: “Pamoja na hali mbaya ya hewa yenye baridi kali, wapiganaji wetu wamemaliza kufanya msako wa usiku baada ya kupewa vifaa maalum vya kutumia kuangalia wakati wa usiku, vinavyo wawezesha kuona bila kutumia taa”. Akaongeza kua: “Hakika opresheni ilikusudia kutumia mazingira magumu kama fursa ya kuwasaka magaidi wa Daesh kwani ndio wakati bora wa kuimarisha ulinzi katika jangwa”.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kilikamilisha jukumu lake katika hatua ya kwanza kwa mafanikio, kilifanya msako katika eneo lenye ukubwa wa kilometa (1750) jangwani, kwa kushirikiana na viongozi wa kikosi cha muungano pamoja na Furatu-Ausat kutimua mabaki ya magaidi wa Daesh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: