Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) leo (19 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (14 Februari 2020m) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai amezungumza vipengele vingi vya ki-akhlaq na kimalezi vinavyo gusa mazingira halisi tunayo ishi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:
- - Misingi ya tabia njema ni jambo la lazima katika sekta zote za maisha ya mtu mmoja mmoja na jamii zote za wanadamu bila kujali kua ni wanadini au sio wanadini.
- - Tabia njema ni msingi muhimu wa mahusiano mema ya jamii na hujenga jamii yenye nguvu.
- - Tabia njema hujenga miamala salama ya kiuchumi isiyokua na dhulma wala ukandamizaji.
- - Tabia njema ni msingi wa utulivu wa nafsi kwa mtu na jamii.
- - Tabia njema ni msingi wa maendeleo ya jamii kwa ujumla.
- - Jamii yeyote isiyokua na tabia njema itakosa nguvu, heshima na maendeleo.
- - Jamii zenye maendeleo ni zile ambazo zinasifika kwa tabia njema.
- - Hatukatai wala hatuna shaka kua wairaqi wana baadhi ya tabia nzuri, kama vile ukarimu, upendo, mapenzi ya dini na taifa.
- - Jambo la kusikitisha kuna mapungufu ya ki-Akhlaq na vitendo vibaya katika jamii zetu, ambavyo lazima tuvikemee na kuviondoa kadri tuwezavyo.
- - Miongoni mwa mambo mabaya katika jamii yetu ni: ubinafsi, nao ni pale mtu anapo jali maslahi yake binafsi, wala hajali maslahi ya wengine na jambo hilo wanalo sana wenye madaraka.
- - Miongoni mwa mambo mabaya katika jamii yetu ni: uongo na unafiki pamoja na kutuhumu watu bila dalili na kujenga mfarakano kijamii na kisiasa.
- - Miongoni mwa mambo mabaya katika jamii yetu ni: ukabila na umadhehebu, ambao unasababisha watu wataifa moja wachukiane kwa misingi hiyo na wala wasisaidiane.
- - Miongoni mwa mambo mabaya katika jamii yetu ni: ni kushambuliana na kuvunjiana heshima hata kama anayeshambuliwa anahudumia taifa na raia.
- - Miongoni mwa mambo mabaya katika jamii yetu ni: kutumia nguvu katika kutatua mizozo ya kifamilia na mingineyo, ambayo inaweza kutatuliwa kwa njia za amani au za kisheria.
- - Miongoni mwa mambo mabaya katika jamii yetu ni: tabia ya rushwa, kufoji, kutakatisha pesa na kupora mali za umma.
- - Miongoni mwa mambo mabaya katika jamii yetu ni: mpasuko wa familia, mmomonyoko wa maadili, utumiaji wa dawa za kulevya, na watu kuiga mambo ya kimagharibi ambayo yako mbali na maadili ya kiiraq.
- - Miongoni mwa mambo mabaya katika jamii yetu ni: ni kulazimisha mtazamo wa mtu binasfi au kundi fulani kua mtazamo wa kila mtu.
- - Miongoni mwa tiba za matatizo hayo ni: kutoa haki inayo stahiki kwa somo la Akhlaq katika shule za msingi, sekondari na vyuo, sawa na masomo mengine ya sekula.
- - Miongoni mwa tiba za matatizo hayo ni: taifa linapokua na mmomonyoko wa maadili au matendo mabaya haifai kunyamaziwa, lazima watu wakemee maovu.
- - Tukizingatia misingi ya tabia njema katika jamii zetu tunaweza kujenga taifa lenye maendeleo.
- - Sio sahihi swala la tabia njema kuwa sawa na kauli mbiu ya kutamkwa mdomoni tu bila kufanyiwa kazi kwa vitendo.
- - Usafi, kufanya kazi kwa bidii na kuoneana huruma ni miongoni mwa tabia njema zinazo takiwa kufanyiwa kazi kwa vitendo.