Kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimekamilisha kutengeneza njia maalum kwa ajili ya gari maalum za kubeba wazee na watu wenye ulemavu, pembezoni mwa barabara inayo elekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) upande wa Kibla, ambayo imepanuliwa hivi karibuni, kazi hiyo ni miongoni mwa vipengele vya kutoa huduma.
Kupangilia misafara ya (kwenda na kurudi pamoja na kusimama) ambapo ni pande mbili za barabara tajwa, upande mmoja zinapita gari za kwenda na mwingine za kurudi, dereva anatakiwa kufuata mipaka iliyo wekwa, njia hizo zinaupana wa mita mbili na nusu barabara yote, huku ukiwa umebaki upana wa mita tano pembeni kwa ajili ya waenda kwa miguu.
Kazi hiyo imefanywa sambamba na kufunga hema za kupumzika mazuwaru na kuwastiri na jua wakati wa kiangazi au mvua wakati wa masika.
Tambua kua Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyake, inafanya kila iwezalo kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya kiroho ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kupunguza usumbufu kwa mazuwaru watukufu.