Katika mazingira ya furaha, Atabatu Abbasiyya tukufu inapokea usiku wa kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Zaharaa (a.s) kwa kufanya hafla kubwa iliyo ratibiwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), alasiri ya Ijumaa mwezi (19 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (14 Februari 2020m), kama sehemu ya harakati zinazo fanywa na kitengo hicho katika kumbukumbu za mazazi na vifo vya maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kuhuisha mambo yao.
Hafla imefunguliwa kwa Quráni tukufu iliyosomwa na Sayyid Badri Mamitha, na kupambwa na vipengele mbalimbali ikiwa ni pamoja na kaswida na mashairi ya kumsifu bibi Zaharaa (a.s) na kutaja historia yake na utukufu wa kufuata mwenendo wake sambamba na kuhuisha utajo wao na mambo yao, na kuingiza furaha katika moyo wa Imamu wao Swahibu Asri wa Zamaan (a.f).
Washairi walipata nafasi ya kushiriki katika halfa hiyo, wameimba beti za kuonyesha mapenzi na utiifu kwa kizazi kitakatifu, walipanda kwenye mimbari mmoja baada ya mwingine, alianza mshairi Ahmadi Madhwi/ kisha kikafuata kikosi cha kaswida kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu, akafuata Mula Ahmadi Shaakir, mshairi Muhandi Hasanawi, Mula Maahir Rikabi, wote waliimba beti za kumsifu mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s).
Hafla ikahitimishwa kwa kuwapa zawadi wahudhuriani pamoja na mazuwaru wa mwezi wa familia Abulfadhil Abbasi (a.s).