Ardhi inan’gaa kwa nuru ya Fatuma (a.s).

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi ishirini Jamadal-Aakhar mwaka wa tano wa utume, ardhi ilin’gaa kwa nuru ya Mola wake kutokana na kuzaliwa kwa Fatuma Zaharaa (a.s) pande ya mtume mtukufu (s.a.w.w).

Shekh Swaduuq (r.a) amepokea kwa sanadi madhubuti kutoka kwa Mufadhil bun Omar anasema: Nilimuuliza Abu Abdillahi (a.s), kuhusu mazazi ya Fatuma (a.s) yalikua vipi? Akasema: Ndio, Khadija alipoolewa na Mtume (s.a.w.w) wanawake wa Maka walimtenga, wakawa hawaendi kwake wala hawamsalimii, akawa mpweke, baada ya kupata ujauzito wa Fatuma (a.s), Fatuma alikua anamzungumzisha na kumuambia avumilie akiwa tumboni mwake, na alikua anamueleza Mtume (s.a.w.w) jambo hilo.

Siku moja Mtume (s.a.w.w) akaingia ndani akamkuta Khadija anaongea na Fatuma (a.s), Mtume akamuuliza: Ewe Khadija unaongea na nani? Akajibu mtoto aliye tumboni mwangu ananiongelesha na kuniliwaza, akasema: ewe Khadija Jibrilu kaniambia kua ni mwanamke mtakasifu, na Mwenyezi Mungu mtukufu atajaalia kizazi changu kiendelezwe na yeye, na atajalia Maimamu katika kizazi chake watakaokua makhalifa katika ardhi baata ya kukatika wahyi wake.

Hali hiyo iliendelea kumtokea bi Khadija hadi alipo pata uchungu, akawaita wanawake (wakunga) wa kikuraishi na bani Hashim waje kumsaidia wakati wa kujifungua, wakakataa na kumuambia kua wewe ulituasi haukusikiliza, ukaolewa na Muhammad yatima wa Abu Twalib fakiri asiyekua na mali, hatuji wala hakuna yeyote atakaekusaidia.

Bibi Khatija (a.s) akafadhaishwa na jambo hilo, ghafla wakaingia wanawake wane warefu kama vile wanawake wa bani Hashim, akashangaa baada ya kuwaona, mmoja wao akasema: ewe Khadija usishangae, Mola wako ametutuma kwako, sisi ni dada zako, mimi ni Sara na huyu ni Asia binti Muzaahim na ndio rafiki yako peponi, na huyu ni Maryam binti Imran na huyu ni Kulthum dada wa Mussa bun Imran, tumekuja kua wakunga wako, mmoja akakaa kulia kwake na mwingine kushoto kwake, wa tatu akakaa mbele yake na wa nne akakaa nyuma yake, kisha akazaliwa Fatuma mtakatifu, baada ya kuzaliwa nuru iliangaza katika nyumba zote za watu wa Maka, na ikaangaza mashariki na magharibi ya dunia, halafu wakaingia mahuraini kumi, kila mmoja akiwa ameshika beseni na birika la maji kutoka peponi kwenye mto wa Kauthar.

Yule mwanamke aliyekua amekaa mbele yake, akachukua maji yale na akamuogesha halafu akachukua vitambaa viwili vyeupe kushinda maziwa na vinaharufu nzuri kushinda miski na ambar, akamfunga kitambaa kimoja na kingine akamfunika kisha akamuongelesha naye Fatuma (a.s) akatamka shahada mbili, akasema: Nakiri kwa moyo na kutamka kwa ulimi ya kwamba hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa haki ispokua Allah na hakika baba yangu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mbora wa Mitume na hakika mume wangu ni mbora wa Mawasii na watoto wangu ni wajukuu bora.

Kisha akawatolea salamu na akamtaja kila mmoja kwa jina lake, wakaanza kucheka kwa furaha, mahuraini pamoja na viumbe wa mbinguni wakaanza kupeana habari ya kuzaliwa kwa Fatuma (a.s), ikaangaza nuru kubwa angani ambayo ilikua haijawahi kushuhudiwa kabla ya siku hiyo, wale wanawake wakasema: Mchukue mtoto wako ewe Khadija hakika huyu ni msafi mtakasifu amebarikiwa yeye na kizazi chake, akamchukua kwa furaha kubwa na kumnyonyesha, makuzi ya bibi Fatuma (a.s) ndani ya siku moja yalikua sawa na makuzi ya mtoto wa kawaida kwa muda wa mwezi mmzima, na makuzi yake ya mwezi sawa na makuzi ya mtoto wa kawaida ya mwaka mzima.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: