Upanuzi wa sehemu ya kupumzikia katika chuo kikuu cha Al-Ameed.

Maoni katika picha
Miongoni mwa mkakati wa ujenzi unaoshuhudiwa katika chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kwenye maeneo mbalimbali, hivi karibuni chuo kimekamilisha ujenzi wa uwanja mpya wa michezo na mpira wa miguu.

Huu ni miongoni mwa miradi ya lazima kwa chuo chochote, uwanja mpya wa wanafunzi unachukua nafasi ya uwanja wa zamani, na uwanja huu umesanifiwa na kujengwa kisasa ukiwa na eneo la kupumzikia.

Uwanja wa mpira wa miguu unaukubwa wa (42x22) mita za mraba, sakafu yake imetengenezwa kwa vifaa vya kisasa kutoka Holandi, mkandarasi wa ujenzi wa uwanja huu ni shirika lenye uzowefu mkubwa katika ujenzi wa viwanja vya michezo vya kisasa, baada ya kutenga eneo maalum tofauti na lile la zamani, uwanja huu utatumika kama moja ya sehemu za kuja kupumzika wanafunzi na kushiriki michezo mbalimbali.

Mradi huu umetekelezwa kwa ajili ya kuwajengea wanafunzi wa chuo mazingira mazuri ya kujisomea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: