Idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya kupitia kamati yake ya kuhuisha matukio ya kidini, imefanya hafla kubwa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wameadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa mbora wa wanawake Fatuma Zaharaa (a.s), na kuhudhuriwa na kundi la mazuwaru wa malalo takatifu na viongozi wa vitengo vya Ataba na watumishi wake.
Hafla ilifunguliwa kwa Quráni tukufu iliyosomwa na Sayyid Mamitha, yakafuata mawaidha yaliyo tolewa na Shekh Ali Mujaan kutoka kitengo cha Dini, akafafanua utukufu wa tukio hili adhim katika nyoyo zetu na kuhuisha mambo ya Ahlulbait (a.s), kama ilivyo pokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) pale alipo sema: (Huisheni mambo yetu Mwenyezi Mungu amrehemu atakaehuisha mambo yetu), akafafanua kwa nini alipewa jina la Fatuma (a.s), akaeleza baadhi ya sifa zake na athari yake katika jamii ya kiislamu.
Baada yake wakafuata washairi waliosoma beti za kumkumbuka na kumsifu bibi huyo mtakasifu, washairi waliopata nafasi hiyo ni: Rafaát Swafi, Maitham Faalih, Ihabu Maalik, na wote wamesoma beti za kuonyesha mapenzi na utukufu wa Batuli Fatuma Zaharaa (a.s).