Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya imefanya mahafali nyingi za usomaji wa Quráni, kupitia matawi yake ya mikoani, kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mbora wa wanawake wa ulimwenguni wa kwanza na wa mwisho Fatuma Zaharaa (a.s).
Ufunguzi wa mahafali hizo ulifanyika katika mji mkuu wa Bagdad kwenye mradi wa semina za Quráni, na kushiriki jopo la wasomaji, hafla nyingine ikafanywa katika wilaya ya Hadhar mkoani Muthanna, na kuhitimisha mahafali hizo katika mji huu mtukufu wa kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), kupitia tawi la Maahadi la Najafu Ashrafu.
Tambua kua Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hufanya mahafali za usomaji wa Quráni tukufu sambamba na matukio ya kidini, kama sehemu ya kuimarisha utamaduni wa kushikamana na mafundisho ya Quráni katika jamii.