Ugeni wa idara ya ustawi wa jiamii chini ya Atabatu Abbasiyya pamoja na mawakibu za kutoa misaada zimetembelea kaskazini ya Baabil/ wilaya ya Musayyib, kusalimia familia za watu walipata shahada kwenye maandamano ya amani yanao ruhusiwa na katiba ya nchi na kuungwa mkono na Marjaa Dini mkuu.
Ustadh Qassim Maamuri amesema kua: “Hakika ziara hii ni kwa ajili ya kutembelea familia za watu waliopata shahada kwenye maandamano ya amani katika mikoa ya kaskazini ya Baabil, kuwapa pole kwa kupoteza wapenzi wao, maeneo yaliyo tembelewa ni (Musayyib, Saddah Hindiyya, Iskandariyya).
Kumbuka kua idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inakaribia kukamilisha ratiba ya kutembelea familia za watu waliopata shahada kwenye maandamano ya amani katika mikoa ya Iraq, kwa sasa kituo cha harakati hiyo kipo kaskazini ya mkoa wa Baabil.