Maji yananyenyekea mbele ya bwana wake.. unaletewa picha na kituo cha uzalishaji na matangazo mubashara Alkafeel.

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na eneo la katikati ya haram hizo zinamuonekano mzuri sana, hususan wakati wa kunyesha mvua na baada yake, jambo linalo wafanya makumi ya wapiga picha pamoja na mazuwaru kupiga picha muonekano huo mzuri wa Ataba mbili na eneo la katikati ya Ataba hizo.

Haidari Jaasim Mankushi mmoja wa wapigapicha wa kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ametumia wakati wa kunyesha mvua katika mji wa Karbala kupiga picha zinazo tuonyesha uzuri wa muonekano unao wavutia maelfu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii, tulipo muuliza siri ya kusubiri wakati huo na kupiga picha hizo amesema: “Ili Ataba zionekane vizuri mbele yangu”.

Akaongeza kusema: “Nimekua nikitafuta wakati mzuri wa kupiga picha zitakazo onyesha eneo kubwa zaidi la Ataba likiwa limeaksiwa na maji, namshukuru Mwenyezi Mungu hilo limetimia, imekua kama nilivyo taka kwa taufiq ya Mwenyezi Mungu na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Baada ya picha hizo kusambaa katika mitandao mbalimbali ya mawasiliano ya kijamii Mankushi amesema: “Lengo langu kuu kuhusu picha hizi ni kuonyesha uzuri wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika muonekano huo kwa kila mtu aliyembali na Ataba hiyo takatifu, aone uzuri wa jengo linapokua limeaksiwa na maji ya mvua, hususan wale wanaoshindwa kuja kufanya ziara kutokana na sababu fulani, nimefurahi sana kusambaa kwa picha hizi”.

Tambua kua mpiga picha bwana Haidari Jaasim Mankushi ni mmoja wa wapigapicha wa kituo cha uzalishaji Alkafeel na matangazo mubashara chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, amesha pata tuzo nyingi kwenye mashindano mbalimbali ya upigaji wa picha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: