Idara ya kilimo katika jengo la Shekh Kuleini yatangaza uzalishaji wa miche ya msimu.

Maoni katika picha
Idara ya kilimo katika jengo la Shekh Kuleini chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuotesha miche mipya inayo endana na hali ya hewa ya Iraq, sambamba na kuendelea kuotesha aina bora za miti ya kivuli na mauwa.

Wataalamu wa idara hiyo wanafanya kazi kila siku ndani ya mwaka mzima, chini ya ratiba maalum, kwa ajili ya kuboresha sekta ya kilimo.

Kutokana na uchache wa miche ambayo huoteshwa wakati wa masika na baada yake, wamefanikiwa kuingiza aina mpya za miche, miongoni mwa aina hizo ni: (miche ya msimu Afwaan), (Qarful Aadi), (Lihana nyeupe na nyekundu) na (Kawakibu).

Tambua kua shamba boy wa jengo la Shekh Kuleini walianza kazi tarehe (1/8/2019m) katika eneo lenye ukubwa wa (mita 200), wametengeneza kitalu kizuri ndani ya nyumba ya vioo kwa ajili ya kuotesha mimea katika ubora wa hali ya juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: