Daru Dhiyafatu Abbasi imepewa jina la Imamu Haadi (a.s).

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Jumamosi (23 Jamadal Aakhal 1441h) sawa na (2 Aprili 2016m) ilizindua mradi wa jengo la wageni la Imamu Haadi (a.s), wakati wa sherehe za kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Fatuma Zaharaa (a.s), jengo hilo linatoa huduma nyingi kwa maelfu ya mazuwaru ndani ya kipindi chote cha miaka minne iliyopita.

Mradi huu unalenga kuongeza idadi ya wageni wanaopewa huduma katika jengo hilo miongoni mwa wale wanaokuja kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya Ataba za Karbala tukufu kua na nafasi kubwa kiroho, kifikra na kitamaduni dunia nzima.

Jengo hilo lipo kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (1000), linaghorofa nane pamoja na tabaka la chini (sardabu), ambapo kuna vyoo (100) vya wanaume na wanawake.

Ghorof la kwanza ni maalum kwa ajili ya kupokea wageni na baadhi ya miundo mbinu kama vile kamera na viyoyozi, ghorofa zingine zinamatumizi tofauti pamoja na vyumba vya kulala (110) vyote vinaukubwa sawa.

Ghorofa la samba ni sehemu ya mgahawa, kuna sehemu ya jiko na ukumbi wa chakula, na ghorofa la mwiso lina kumbi mbili za mikutano pamoja na mambo mengine ya utowaji wa huduma.

Mradi huu ulitekelezwa na shirika la ujenzi la Karbala Twayyibah chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: