Tutashinda vipi mitihani?

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye mradi wa (mbeba ujumbe wa Zainabiyya) imeandaa warsha isemayo (kushinda mitihani), na kualika wanafunzi kufuatia kuanza kwa mitihani ya nusu mwaka.

Makamo kiongozi mkuu wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya Ustadhat Taghridi Abdulkhaaliq Tamimi, ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu warsha hiyo: “Ratiba ya kila wiki ya mradi wa (mbeba ujumbe wa Zainabiyya) inavipengele vingi, kuna ufanyaji wa warsha ya kila wiki ya wanafunzi wa sekondari, kutokana na kuanza mitihani ya nusu mwaka, warsha inahusu namna ya kujizuwia kupaniki (kufadhaika) ndani ya chumba cha mtihani, jambo ambalo husababisha mwanafunzi ashindwe kujibu vizuri”.

Akabainisha kua: “Warsha hii inaongozwa na Mhadhiri Abdulkarim kwa namna rahisi kueleweka na wanafunzi, ili kufikia malengo na kujiepusha na baadhi ya changamoto za mitihani, akafafanua tofauti ya kujisomea na kufanya mtihani kwa usahihi, akasema kua wanachuoni wamewagawa wanafunzi katika makundi matatu, kuna wanaojisomea vizuri na kufanya mtihani vibaya, kundi la pili hawajisomei vizuri lakini wanafanya vizuri mitihani yao, na kundi la tatu wanajisomea vizuri na wanafanya mitihani vizuri, ndio kundi linalo takiwa”.

Mwisho wa warsha ikatolewa nafasi ya kujadiliana baina ya wanafunzi na mkufunzi, ambapo aliwajibu maswali yote na kutoa ufafanuzi zaidi pale ulipo hitajika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: