Hospitali ya rufaa Alkafeel imekusudia kufanya kongamano la pili kwa ajili ya kuwazawadia wadau wa matibabu.

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel imekusudia kufanya kongamano la pili la kuwazawadia wadau wa matibabu hapa nchini chini ya Atabatu Abbasiyya siku ya Ijumaa ijayo (21 Februari 2020m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kongamano la kwanza lilifanywa na uongozi wa Hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya mwaka jana, na wadau wa matibabu kadhaa wakapewa zawadi.

Hii ni kuonyesha thamani ya mchango wa kuhudumia binaadamu unaotolewa na mhusika, na kuwakumbusha kua wao ni watu muhimu, na wataendelea kukumbukwa kwa wema kizazi hadi kizazi kutokana na kazi wanazo fanya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: