Kituo cha utamaduni wa familia charatibu mhadhara kuhusu maisha ya mwanamke

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa mwanamke chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeratibu mhadhara kuhusu maisha ya mwanamke ndani ya ukumbi wake, mhadhara huo unaitwa (uendeshaji wa maisha ya mwanamke), jambo hilo linalenga kuboresha uwezo wa mwanamke katika kupambana na changamoto za maisha zinazo tishia wanafamilia na utulivu wa nafsi.

Mhadhara huo pia umejikita katika kutambulisha zana muhimu na njia za kupata utulivu katika maisha na kutengeneza mazingira mazuri kwa watoto, jambo hili ni miongoni mwa harakati za kuboresha utamaduni wa maisha wa mwanamke wa kiislamu na muendelezo wa mihadhara ya kielimu.

Kumbuka kua kituo cha utamaduni wa familia, ni moja ya vituo vinavyo angalia utamaduni wa familia na jamii, ofisi zake zipo Karbala/ mtaa wa Mulhaq/ barabara ya Hospitali ya Hussein (a.s)/ jengo la kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s). Kwa maelezo zaidi piga simu namba (07828884555).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: