Idara ya mafunzo imeandaa semina ya: (Mfumo wa utafiti katika historia ya kiislamu).

Maoni katika picha
Idara ya mafunzo katika kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu imeratibu semina yenye anuani isemayo (Mfumo wa utafiti katika historia ya kiislamu) kwa walimu wa shule za Alkafeel wapatao (30) wakiwemo walimu wakuu na walimu wa kawaida.

Mkufunzi wa semina Ustadh Karaar Hussein Ma’muri ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: semina ilikua na mihadhara tisa inayo husu mfumo wa utafiti katika historia ya kiislamu, mhadhara wa kwanza ulikua unahusu mafuhumu ya mfumo wa utafiti, wa pili: muundo wa utafiti katika historia ya kiislamu, wa tatu: utangulizi wa utafiti na kubaini rejea, wa nne: kuchagua mada za utafiti, wa tano: kuweka mikakati ya utafiti, wa sita: kukusanya fifaa vya kielimu.

Akongeza kua: mhadhra wa saba: namna ya kunukuu kutoka kwenye rejea na kuandika kwenye karatasi, au zana unayo tumia kukusanya taarifa, mhadhara wa nane: namna ya kutumia vitabu rejea na namna ya kuandika nakala pamoja na namna ya kubadilisha kutoka katika jina la Muandishi na kua jina kamili, na kifo cha muandishi wake pamoja na kutaja namba ya toleo, sehemu kilipo chapishwa, idadi ya juzuu na kurasa, mhadhara wa mwisho ukahusu namna ya kuandika maazimio na maswali na majibu.

Wakahitimisha kwa: kutaja maazimio muhimu likiwemo azimio la kuingiza somo ya utafiti wa kihistoria katika ratiba ya masomo ya darasa la tano katika shule za wasichana Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: