Idara ya maraya na mapambo imeanza kupamba haram tukufu

Maoni katika picha
Mafundi wa idara ya maraya na mapambo chini ya kitengo cha usimamizi wa haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wameanza kazi ya kukarabati maraya na mapambo ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na milango ya haram tukufu na sehemu mpya iliyo ongezwa, wanafanya hivyo kwa ajili ya kulinda uzuri wa maraya na mapambo ya malalo takatifu ya mnyweshaji wenye kiu Karbala (a.s).

Kiongozi wa idara ya maraya na mapambo Ustadh Hashim Ayubu Hashim amesema kua: “Mafundi wa idara wanaujuzi wa hali ya juu, wanasafisha maraya na mapambo ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa umakini mkubwa, wanatengeneza upya sehemu zilizo haribika, na kuhakikisha zinakua na muonekano mzuri”.

Akaashiria kua: “Kazi ya ukarabati inahusisha kufungua mapambo na kubadilisha taa zilizo haribika”.

Akasema: “Kazi ya usafi ni pamoja na kuondoa vumbi kwenye mapambo na maraya na kurekebisha sehemu zilizo haribika, tunatumia zana maalumu kusafishia vioo, pamoja na kutumia winchi kwa ajili ya kufikia sehemu za juu ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akasisitiza kua: “Kazi hii hufanywa ndani ya kipindi cha mwaka mzima, kwa ajili ya kutunza usafi na kulinda uzuri wa maraya na mapambo ya haram tukufu, watumishi wa idara hiyo wanafanya kazi muda wote bila kuchoka”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: