Kitengo cha maadhimisho kinatoa zawadi kwa wanafunzi waliopata ushindi kwenye shindano la uchoraji.

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya jumatano ya mwezi (24 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (19 Februari 20202m), kimewapa zawadi wanafunzi walioshinda kwenye shindano la uchoraji la watoto wenye umri wa chini ya miaka kumi, ambalo hufanywa kila mwaka wakati wa msimu wa huzuni za Fatwimiyya katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Hafla ya kugawa zawadi imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya na kuhudhuriwa na rais wa kitengo hicho bwana Riyadh Na’mah Salmaan, na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Dokta Ahmadi Swabihi.

Zawadi hizo ni sehemu ya kuwashajihisha na kuwashawishi watoto wengine wajitokeze kushiriki mwaka ujao na wapate nafasi za kwanza, shindano hili linalenga kuingiza mapenzi ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika nyoyo za watoto wadogo, na kuwafanya wafuate mwenendo wao na wajue dhulma walizo fanyiwa kwa miaka mingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: