Multaqal-Qamaru yapokea vijana 80 kutoka Bagdad

Maoni katika picha
Multaqal-Qamaru yapokea vijana (80) kutoka Bagdad waliokuja kushiriki kwenye kongamano hilo.

Wasimamizi wameandaa ratiba kamili kwa vijana wanaoshiriki yenye mihadhara na nadwa zinazo husu sekta tofauti za elimu na utamaduni, sambamba na vipindi vya mapumziko ambavyo watatembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya.

Mkuu wa Multaqal-Qamaru Shekh Harith Daahi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Katika ratiba ya Multaqal-Qamaru leo tumepokea vijana (80) kutoka mikoa tofauti”.

Akaongeza kua: “Vijana hao wamepatikana kutokana na mawasiliano ya Atabatu Abbasiyya katika mikoa yao, tunatarajia kua watasoma kwa bidii na kuongeza ujuzi wao”.

Akaendelea kusema: “Baadhi ya vijana wanaoshiriki ni wanaharakati wakubwa wa kulinda usia wa Marjaa Dini mkuu aliotoa kwa vijana, na sisi tunaendelea kuandaa semina, warsha na nadwa kwa vijana wanaotumikia jamii ya wairaq”.

Akafafanua kua: “Vijana hao watakaa siku tatu na watapewa mafundisho mbalimbali pamoja na kutembelea miradi ya Ataba, warsha inahusu mambo matatu muhimu, jambo la kwanza ni kua na msimamo katika Dini, nalo ni jambo muhimu litakalo hutubiwa wakati wote, jambo la pili ni kujiendeleza na jambo la tatu ni mwenendo wa utamaduni na maendeleo ya vyombo vya habari pamoja na njia za kujadiliana na kujibu shubuha na mengineyo”.

Kumbuka kua Multaqal-Qamaru ni kongamano la kielimu linalo lenga kupambana na changamoto za kidini, kitamaduni na kijamii, pamoja na kuzitafutia majibu kwa njia ya elimu bila chuki wala vurugu ambazo huleta madhara makubwa katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: