Marjaa Dini mkuu aitaka sekta ya afya ifanye kila iwezalo kuwalinda wananchi na taifa na virusi vya “Korona” na ijipange haraka kwa hilo.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ameitaka sekta ya afya hapa Iraq ifanye kila iwezalo kupambana na hatari ya virusi vya Korona, ameyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) leo mwezi (26 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (21 Februari 2020m), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

Bila shaka mnatambua maradhi yanayo tishia dunia kwa sasa ambayo ni virusi vya Korona, tunamuomba Mwenyezi Mungu alinde wananchi na taifa kwa ujumla.

Sekta ya afya wanajukumu la kubainisha hatari ya virusi hivyo na njia ya kujilinda navyo.

Tunatoa wito kwa taasisi za afya lazima ziwe na mkakati madhubuti wa kupambana na tatizo hili, ni vizuri kubaini tatizo kisha kuangalia namna ya kulitatua.

Maandalizi tunayotaka lazima yaendane na ukubwa wa tatizo, tunamuemba Mwenyezi Mungu atulinde, lakini tusisahau kauli isemayo (Kinga ni bora kuliko tiba), lazima tuwe makini na kuchukua tahadhari, tunatoa wito kwa sekta ya afya ifanye kila iwezalo kuwalinda raia na taifa kutokana na virusi hivyo hatari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: