Katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) leo mwezi (26 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na tarehe (21 Februari 2020m), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ameongea nukta nyingi za kimalezi na kimaadili zinazo husu mazingira halisi tunayo ishi kwa sasa, miongoni mwa nukta hizo ni:
- - Mtu aliye changanikiwa ni yule asiejua ukweli wa mambo.
- - Tunatofautiana katika njia za kuthibitisha mambo tunayo yajua.
- - Mtu yeyote anapokua na msimamo au anapo amini jambo anahitaji kua na vielelezo au dalili zitakazo mfanya asibabaishwe na jambo lolote.
- - Kuna tukio linawakilisha haki na kuna mtu kachanganikiwa hajui ni haki au batili.
- - Hutokea baadhi ya watu wakachanganikiwa katika kuitambua haki wakati inapotokea fitina.
- - Imamu (a.s) ametaja mzani wa kutumia katika kujua haki na mwenye nayo.
- - Sio sawa kufuata jambo bila ushahidi au hoja.
- - Hauwezi kujua haki kwa kuangalia watu.
- - Heshima ya mtu ni kuitambua haki kwa sababu ataweza kumtambua mwenye haki hususan anapokuwepo anaedai yupo kwenye haki.
- - Njia isiyofaa ni kumfuata mtu anaedai yupo kwenye haki kwa kuangalia mtu bila kuangalia haki.
- - Njia inayo faa ni kuitambua haki kisha ndio utambue mwenye haki.
- - Haki inamisingi yake na watu wake tofauti na wale wanaodai haki kwa maslahi yao.
- - Mtu kulinda nafsi yake na kubaini uongo wa mtu anaedai haki ni jambo la lazima.
- - Njia ya kutambua haki inahitaji uwe na msimamo na uwezo wa kubainisha kati ya haki na batili.
- - Kukosa msimamo kunatokana na kukosa kuijua haki na wenye haki.
- - Umuhimu wa kujua haki na batili ni sawa na umuhimu wa kujua dawa na sumu.
- - Lazima mtu aweze kutofautisha kati ya haki na batili, na ashikamane na haki hatakama watakua wachache.
- - Ugonjwa unaotisha dunia ujulikanao kama Korona ni ugonjwa hatari.
- - Sekta maalum ndio wenye jukumu la kutaja hatari na njia za kujilinda na kujitibu.
- - Tunaziomba taasisi za afya zitafute njia nzuri ya kujilinda na maradhi hayo.
- - Mwanaadamu anapoona tatizo anatakiwa alibaini na alitatue.
- - Maandalizi ya kujilinda na maradhi hayo lazima yaendane na ukubwa wa tatizo.
- - Tunatoa wito kwa wenye mamlaka wafanye kila wawezalo katika swala hilo.