Atabatu Abbasiyya tukufu yatangaza kufanya kongamano la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya sita.

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kufanya kongamano la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya sita mwezi mosi Rajabu chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir (a.s) mlinda ujumbe na hazina ya uimamu).

Mjumbe wa kamati ya maandalizi na rais wa kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri amesema kua: “Kongamano litafanywa kwa mwaka wa sita mfululizo, kwa kushirikiana na kitengo cha Dini, kamati ya maandalizi imeshafanya vikao vingi kwa ajili ya kuandaa kongamano la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya sita, kwa ajili ya kujadili ratiba ya kongamano na mada zitakazo wasilishwa ili ziendane na malengo ya kongamano, linalo tarajiwa kufanywa mwanzoni mwa mwezi wa Rajabu 1441h.

Akaongeza kua: “Kamati inayo simamia kongamano imesisitiza vipengele muhimu vya kielimu vinavyo endana na yule ambae kongamano linafanywa kwa ajili yake, na huu ndio mzigo mkubwa kwa kamati ya maandalizi, kwani Imamu Baaqir (a.s) ndio kinara wa kulinda upotoshaji wa Imani na fikra.

Akasema: Miongoni mwa malengo ya kongamano hili ni kufikisha ujumbe kwa kila mfuasi anaeweza kutambua nuru na uzito wa ujumbe tulioachiwa umma huu wa vitu ambavyo tukishikamana navyo hatutapotea milele.

Tambua kua kongamano linavipendele vingi, kuna dama za masomo ya kihauza na kisekula, kuna vikao vya usomaji wa Quráni na mashairi, kongamano hili linafanywa kwa kushirikiana na kitengo cha utamaduni na mambo ya Dini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: