Washiriki wa madarasa ya kufuta ujinga wanafanya mitihani ya nusu mwaka

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu miongoni mwa ratiba zake za (Juudul-Kaafil) yenye harakati mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kusimamia mitihani ya nusu mwaka ya darasa la kufuta ujinga lililofunguliwa mwaka huu.

Kiongozi wa kituo hicho bibi Asmahani Ibrahim amesema kua: “Ufunguzi wa darasa hili unatokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya katika mkakati wa kutoa elimu, unaolenga kupunguza wasiojua kusoma na kuandika katika jamii ya wanawake, hiyo ndio sababu kubwa ya kufungua darasa hili na leo tumefika katikati ya safari kwa kufanya mtihani huu”.

Akaongeza kua: “Tumeandaa sehemu maalumu ya kufanyia mitihani, ambayo inasimamiwa na wakufunzi wenyewe, wenye uwezo na uzowefu mkubwa wa kufundisha kusoma na kuandika”.

Kumbuka kua masomo ni endelevu, wanasomesha siku mbili kwa wiki, ambazo ni Jumapili na Jumatano, kituo kimetoa wito kwa wanaotaka kujiunga na masomo hayo pamoja na mengine wapige simu namba: (07828884555) namba hiyo pia inapatikana kwenye mitandao ya kijamii (viber, whatsap, telegram), au jiunge katika kituo cha utamaduni wa familia kupitia link ifuatayo: https://t.me/thaqafaasria1

Usafiri wa kwenda na kurudi upo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: