Tambua maboresho yaliyo fanywa katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f)

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi matukufu na milango mitakatifu katika Atabatu Abbasiyya wamemaliza kazi ya kufunga dirisha la Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) na kuchukua nafasi ya dirisha la zamani, ambalo linamakumi ya miaka tangu litengenezwe, hivyo kuonekana limechakaa na kutoendana na maboresho yaliyofanywa katika Maqaam hiyo.

Dirisha jipya ambalo limefungwa ndani ya moja ya kumbi za Maqaam, limekamilisha kazi ya mafundi wa Ataba wanayo fanya kwenye Maqaam hiyo, ambayo hupokea Malaki ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq, bado ukarabati unaendelea kuhakikisha eneo hili linakua na muonekano mzuri zaidi.

Rais wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi matukufu Sayyid Naadhim Ghurabi, ametuambia wasifu wa dirisha hilo, amesema kua: “Kwa baraka za mwenye Maqaam takatifu na Abulfadhil Abbasi (a.s) tumekamilisha kazi zote zinazo husu dirisha takatifu, lililotengenezwa kwa ufundi na uhodari wa hali ya juu, limetengenezwa kisasa tena kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) upande wa nakshi na mapambo, linasehemu za mbao na madini kama ifuatavyo:

 • - Urefu wa dirisha ni (mita 6) na kimo (mita 3.5) takriban.
 • - Dahabu halisi iliyotumika katika kutengeneza dirisha hilo inakaribia (kg 1.150).
 • - Madini ya fedha karibu (kg 88).
 • - Madini ya mina za kioo cha bluu (kg 30).
 • - Silva zaidi ya (kg 500) takriban.
 • - chuma kigumu zaidi ya (kg 1.500).
 • - Mbao zilizo tumika ni aina ya Burumi ambazo ni nzito na imara zaidi”.

Akaongeza kua: “Muonekano wa dirisha unapambwa na:

 • - Milango mitano ya dirisha inayo tenganishwa na mlango mmoja wenye sehemu mbili wenye ufito wa maandishi ya watengenezaji na mwaka ulio tengenezwa.
 • - Juu ya milango ya dirisha kuna ufito wa maandishi wenye urefu wa (m 6.6) na kimo cha (sm 19.5) umeandikwa beti za mashairi zisemazo (Ewe mtoto wa Mtume nani anaeitwa kwa jina lako ** mtoto wa Hatwim na Zamzam na mtoto wa Swafa) kuna beti moja juu ya kila mlango wadirisha, kati ya ubeti na mwingine kuna neno (Yaa hujjatu Llah) vitenganisho hivyo viko sita.
 • - Katikati ya mlango wa dirisha na mwingine pametenganishwa kwa nguzo yenye mapambo.
 • - Juu ya ufito wa maandishi kuna ufito wa mapambo wenye urefu wa (mita 6.6) na kimo cha (sm 32) yaliyotiwa naksi za mimea na aya isemayo: (Tunataka kuwaneemesha wale waliodhofishwa katika ardhi na tuwafanye kua viongozi na tuwafanye kua warithi), pembezoni mwake kumeandikwa aya zingine mbili, halafu kuna manene yasemayo (Baqiyatullahi khairun lakum inkuntum mu-uminina) yamezungushiwa mapambo mazuri ya mina ya bluu.
 • - Kuna ufito wa maandishi ya kuanzia aya ya 100 kutoka surat Yunusi isemayo (Haikua nafsi ni yenye kufa…) hadi aya ya 103 isemayo (Hivyo ni haki yetu kuwaokoa waumini) aya hizo zipo juu ya ufito wa dhahabu.
 • - Muonekano wa dirisha unahitimishwa na mapambo (20) ya mauwa yaliyotiwa dhahabu kati ya kila uwa na lingine kuna taa”.

Akaongeza kua: “Umbo la dirisha limefungwa taa zilizo unganishwa na kituo kikuu cha umeme wa dharura, sambamba na taa za rangi ambazo huwashwa kulingana na matukio”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: