Yamesemwa hayo katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye ratiba ya Multaqal-Qamaru Athaqafiy, ambalo ni miongoni mwa harakati za kijana mzalendo wa Alkafeel, inayo simamiwa na idara ya mahusiano ya vyuo katika Ataba tukufu, wanafunzi hao walikua na ratiba ya siku mbili yenye vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:
- - Kutembelea malalo mbili ya Imamu Hussein na Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kutembelea baadhi ya miradi.
- - Kusikiliza mada zilizo tolewa na Shekh Haarith Daahi kiongozi wa kituo cha Multaqal-Qamaru Athaqafi, kuhusu maendeleo, kujitegemea na kujiamini.
- - Kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya, ikiwa ni pamoja na shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud na mashamba ya Khairaatu Abulfadhil Abbasi (a.s), na Darul-Kafeel ya uchapaji na usambazaji, na kiwanda cha maji Alkafeel, pamoja na hospitali ya rufaa Alkafeel.
Wageni walipata fursa ya kusikiliza maelezo kuhusu miradi hiyo na malengo ya kuanzishwa kwake, pamoja na mchango wake katika kuingiza fani mpya kulingana na aina ya mradi.