Nadwa kuhusu virusi vya (Korona) na namna ya kujikinga navyo

Maoni katika picha
Idara ya tiba katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya nadwa kuhusu virusi vya Korona na maradhi ya kuambukiza, kwa ajili ya kuwajengea uwelewa watumishi wake kuhusu hatari ya virusi hivyo na jinsi ya kujikinga, ikiwa ni sehemu ya kuchukua tahadhari na kuwalinda watumishi wa malalo tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru, vilevile ni kufanyia kazi kauli isemayo (kinga ni bora kuliko tiba) na kufuata maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kuchukua tahadhari.

Nadwa imefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Ataba tukufu Alasiri ya Jumapili (28 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (23 Februari 2020m) na kuhudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar na marais wa vitengo vya Ataba pamoja na wawakilishi wa idara ya afya ya Karbala na shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa na viwanda Khairatil-Juud.

Nadwa hiyo ilikua na mada tatu, watoa mada walikua ni:

  • - Dokta Usama Abdulhassan kiongozi wa idara ya tiba katika Atabatu Abbasiyya, alizungumzia mtazamo wa idara kuhusu utendaji wa vitengo vya Ataba katika kutekeleza maelekezo ya afya na kujikinga na kirusi hicho (Korona), kulingana na utendaji wa kila kitengo na muingiliano wake na mazuwaru, kuna vitengo ambavyo hufanya kazi moja kwa moja na mazuwaru, akabainisha mambo ambayo wanatakiwa kufanya kwa ajili ya usalama wao na mazuwaru, pamoja na maelekezo yaliyo tolewa na wizara ya afya ya Iraq ambayo yamesambazwa kwa watumishi wote ili wayafanyie kazi, pia kuna ripoti zinatolewa kila siku kuhusu swala hilo.
  • - Dokta Salaam Swahibu Abedi muwakilishi wa idara ya afya ya Karbala, ameeleza baadhi ya tahadhari zilizofanywa na wizara ya afya ya Iraq, kwa ajili ya kujikinga na kirusi hicho kama ikitokea –Allah atuepushie- tunamshukuru Mwenyezi Mungu hadi sasa hakijatokea, akasisitiza kua haijaripotiwa taarifa yeyote ya maambukizi ya kirusi hicho hapa Iraq, kisha akaeleza kuhusu kirusi hicho na sababu za kupatikana kwake pamoja na mbinu za kupambana nacho na matibabu yake.
  • - Dokta Ali Mussawi kutoka shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa na viwanda Khairatul-Juud, ameeleza mafanikio makubwa waliyopata katika uzalishaji wa shirika hilo, ambalo linapambana kutafuta kinga ya kirusi hicho na kupunguza maambukizi yake –Allah atuepushie- miongoni mwa kinga za virusi hivyo ni kutumia sabuni ya maji na aina zingine za visafishio ambavyo hutumika sehemu tofauti, kama vile nyumbani na sehemu zingine, na vimeonyesha mafanikio makubwa ya kuuwa bakteria.

Mwisho wa nadwa hiyo ukafunguliwa mlango wa maswali na majibu kuhusu mada zilizo wasilishwa, watoa mada walijibu maswali na kufafanua zaidi pale palipo hitaji ufafanuzi zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: