Kama kawaida; Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum katika mwezi huo, miongoni mwa vipengele vya ratiba hiyo ni:
- 1- Kuweka mazingira ya furaha na mapambo maalum katika kuadhimisha mazazi yaliyotokea katika mwezi wa Rajabu Aswabu.
- 2- Kufanya hafla kadhaa ndani ya haram tukufu ya Abbasi katika siku za kukumbuka mazazi, kwa kuanzia na hafla ya kuzaliwa kwa Imamu Baaqir (a.s) itakayo fanywa jioni ya leo, sambamba na hafla zingine zitakazo fanywa kwa ajili ya kuhuisha kuzaliwa kwa nuru za Muhammadiyya katika mwezi huu mtukufu, ikiwemo kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s).
- 3- Kufanya kongamano la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya sita kuanzia siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Rajabu Aswabu chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir –a.s- ni mlindaji wa Utume na hazina ya Uimamu) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s).
- 4- Kujiandaa kupokea mazuwaru watakao kuja kufanya ziara ya Rajabiyya ambayo ni maalum kwa bwana wa mashahidi (a.s) usiku wa mwezi kumi na tano kutoka miji na nchi tofauti.
Kumbuka kua mwezi wa Rajabu Aswabu unamatukio mengi ya kidini, kuanzia kuzaliwa kwa Imamu Baaqir, kuzaliwa Imamu Jawaad, kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), pamoja na kifo cha bibi Hauraa Zainabu mtoto wa kiongozi wa waumini (a.s).