Mafundi wa kitengo cha haram mbili tukufu wameanza kutengeneza moja ya barabara za mji mkongwe.

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu, wanafanya matengenezo maalum ya moja ya barabara iliyopo mji mkongwe katika eneo la mlango wa Bagdad (Baabu-Bagdad).

Matengenezo hayo yanahusisha upanuzi wa barabara hiyo na kuweka lami mpya, pamoja na kujenga mitaro ya maji, na kutengeneza sehemu zote zilizo haribika kwenye barabara hiyo. Aidha wanachambulia miti iliyopo barabarani na kuondoa iliyodumaa kisha kupanda mingine mizuri kwa ajili ya kupendezesha barabara.

Kazi hiyo ipo ndani ya mkakati wa kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu, unaolenga kukarabati mji mkongwe, kwa kutengeneza barabara za zamani zinazo elekea katika uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu.

Kumbuka kua kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya ni sawa na vitengo vingine, kinafanya kazi kubwa kwa ajili ya kuwahudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: