Wasimamizi wa haram tukufu wameanza kutekeleza mkakati wa kujilinda na maradhi ya Korona.

Maoni katika picha
Kama sehemu ya kuchukua tahadhari na kufanyia kazi kauli isemayo (kinga ni bora kuliko tiba), idara ya uangalizi wa haram na kitengo cha uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), zimeanza kutekeleza mkakati wa kujikinga na maradhi ya (Korona), ukizingatia wao hufanya kazi moja kwa moja na mazuwaru, chini ya utaratibu wa mkakati uliowekwa na idara ya tiba katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Tahadhari zinazo chukuliwa kwa sasa asilimia kubwa ni kuongeza umakini, kutokana na mazingira pamoja na kuandaa zana za kujikinga na maradhi hayo.

Kiongozi wa idara ya uangalizi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), Shekh Zainul-Aabidina Adnani Ahmadi Quraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: Idara yetu inajukumu la kuwahudumia mazuwaru na kuratibu matembezi yao pamoja na kazi zingine ndani ya haram tukufu, miongoni mwa mambo tuliyo fanya chini ya maelekezo yaliyo tolewa ni:

  • - Kutumia kifaa cha kujikinga (micro safe) na kunyunyizia dawa kwenye dirisha takatifu isiyodhuru madini wala mazuwaru, ambayo imetengenezwa na shirika la Khairatul-Juud na imeoshesha mafanikio yake.
  • - Kufuta mazulia ya haram kwa visafishio maalum.
  • - Kuweka marashi yenye uwezo wa kuuwa bakteria ndani haram ya Abulfadhil Abbasi na maeneo yanayo izunguka, marashi ambayo ni rafiki kwa mazingira na hayaudhi mazuwaru.
  • - Kufungua madirisha ya haram muda wote kwa ajili ya kuingiza hewa mpya na mionzi ya jua”.

Akabainisha kua: “Tumeweka utaratibu maalum ambao hautatizi shughuli zingene zinazo endelea ndani ya haram tukufu.

Kitengo cha usimamizi wa haram pia kimechukua hatua kadhaa za tahadhari, amezieleza kwa ufupi bwana Haadi Hanuun kama ifuatavyo:

  • - Kupunguza misongamano ya mazuwaru katika maeneo ambayo mara nyingi huwa na misongamano.
  • - Kusafisha na kupuriza dawa za kuuwa bakteria kwenye madirisha ya nje katika haram tukufu.
  • - Kuosha matandiko yanayo tumiwa na mazuwaru kila siku.
  • - Kuosha mazulia yaliyo tandikwa ndani ya haram kila siku.
  • - Kufungua hema zilizopo juu ya paa kwa ajili ya kuruhusu mwanga na mionzi ya jua kuingia.

Kumbuka kua mambo hayo ni sehemu ya hatua nyingi za tahadhari zilizo chukuliwa kwa ajili ya kujikinga za virusi vya (Korona) kwa watumishi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: