Kuhuisha mazazi ya Maimamu wawili Baaqir na mjukuu wake Alhaadi (a.s).

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu jioni ya Jumanne (29 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (24 Februari 2020m) imefanya hafla ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Muhammad Baaqir na Imamu Ali Alhaadi (a.s).

Kamati ya kuhuisha matukio ya kidini chini ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ndio walio simamia na kuratibu hafla hiyo, iliyohudhuriwa na watumishi pamoja na mazuwaru watukufu, ilifunguliwa kwa Quráni tukufu kisha Shekh Ali Muhani akapanda kwenye jukwaa na akazungumza kuhusu kuzaliwa kwa maimamu hao wawili (a.s).

Baada yake wahudhuriaji wakapata nafasi ya kusikiliza mashairi yanayo husu Ahlulbait (a.s), yaliyo somwa na Muhammad Faatwimiy, Haidari Shibani, Alaa Isawi na Farasi Asadi, wote walisoma beti za kuonyesha mapenzi na utiifu kwa Ahlulbait (a.s).

Kumbuka kua idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya huadhimisha matukio ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), na imeandaa kamati maalumu kwa ajili hiyo, inayo jumuisha watumishi wa Imamu Hussein (a.s) pamoja na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: