Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kongamano la sita la Imamu Baaqir (a.s) chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir –a.s- ni muendelezaji wa mafundisho ya utume na hazina ya uimamu) ambalo ni sehemu ya kusherehekea kuzaliwa kwake (a.s).
Asubuhi ya Jumanne (25 Februari 2020m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) na kuhudhuriwa na wageni wengi pamoja na viongozi wa kidini na kijamii, wakiwemo wawakilishi wa Ataba na mazaru takatifu.
Kongamano limefunguliwa kwa Quráni rukufu, halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq kisha ukasomwa wimbo wa taifa la Iraq na ule wa Atabatu Abbasiyya, ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya uliosomwa na rais wa kitengo cha Dini Shekh Aadil Wakili, akawaomba waandishi waendelee kuandika mambo yanayohusu maimamu na watu wa nyumba ya Mtume (a.s), pamoja na kuwaenzi wanachuoni walio fuata mlengo wao.
Baada ya hapo mshairi bwana Aadil Swawiri akaburudisha masikio ya wahudhuriaji kwa kusoma shairi lililo muelezea Imamu na utukufu wake.
Kikafuata kikao cha mada ya kwanza iliyokua ikisema (Imamu Baaqir –a.s- ni nguzo miongoni mwa nguzo za Dini ya Mwenyezi Mungu) iliyo wasilishwa na Shekh Ali Mujaan.
Halafu ukafunguliwa mlango wa maoni na maswali, ambapo Shekh alijibu na kutoa ufafanuzi zaidi pale ulipo hitajika, kikao hicho kikafungwa kwa mada hiyo huku mada zingine zikitarajiwa kutolewa alasiri ya leo.