Kikao cha kongamano la Imamu Baaqir (a.s) lililo anza Jumanne (25 Februari 2020m) chini ya kauli mbiu isemayo (Imamu Baaqir –a.s- muendelezaji wa mafundisho ya utume na hazina ya uimamu), kimefunguliwa na mada iliyo tolewa na Shekh Ali Mujaan kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu isemayo: (Imamu Baaqir (a.s) ni nguzo miongoni mwa nguzo za Mwenyezi Mungu) ambapo ameongea kwa ujumla.
Mada hiyo aliigawa sehemu tatu kama ifuatavyo:
Sehemu ya kwanza: Amezungumzia hekima ya kiungu katika maswala ya kuongoa, akasema kua hekima ya Mwenyezi Mungu katika swala hilo inatokana na upole wake, hivyo lazima awawekee waja wake kila kitu kinacho weza kuwasaidia katika kuwafikisha kwenye ukamilifu, kuna mambo mengi ambayo Mwenyezi Mungu amempa mwanaadamu, miongoni mwa mambo hayo ni kuletwa kwa Mitume, (a.s) halafu akawapa mawasii, hakika jambo hilo ni hekima ya Mwenyezi Mungu, yaliyo fanywa na Maimamu (a.s) yanamchango mkubwa, ukizingatia kua wao wenyewe ni sehemu ya mpango wa Mwenyezi Mungu, kila mmoja anatekeleza jukumu lake maalum, hakuna Imamu hata mmoja akiwemo Imamu Baaqir (a.s) ambae yuko nje ya mfumo.
Sehemu ya pili: Athari ya Imamu Baaqir (a.s) katika sekta ya Aqida, taifa lilikua na siasa za kijinga katika zama zake, Imamu (a.s) alijitahidi kulinda utambulisho wa mwislamu halisi uliokua umesimama juu ya mambo mawili ya msingi, kumtawalisha kiongozi wa waumini (a.s) na kujitenga na maadui zake, Imani haiwezi kukamilika ispokua kwa vitu hivyo viwili, Albara-ah na Al-Imaamah.
Sehemu ya tatu: Amezungumzia athari ya Imamu (a.s) katika fiqhi, watu wa zama zake walikua wanafuata mlengo wa ujinga, akawafundisha ibada sahihi ya Hijja, Swala na mambo ya haram, hadi wakawa wanamtolea ushahidi, Imamu (a.s) alifanya kazi ya kuwaongoa watu kupitia madrasa kubwa aliyo fungua.
Kikoa kikafungua mlango wa maoni na maswali kutoka kwa wahudhuriaji, nao waliuliza kwa wingi na wakatoa maoni mbalimbali, naye mtoa mada alijibu maswali na kutoa ufafanuzi zaidi pale ulipo hitajika.