Chuo kikuu cha Alkafeel chaweka darasa mjadala kuhusu kirusi cha Korona.

Maoni katika picha
Kitivo cha tiba na afya katika chuo kikuu cha Alkafeel, kimefanya darasa mjadala kuhusu kirusi cha Korona na maambukizi yake, na njia za kujikinga na kirusi hicho, kwa lengo la kuwajengea uwelewa wanachuo kuhusu kirusi hicho na namna ya kujilinda nacho, darasa hilo limehudhuriwa na idadi kubwa ya wakufunzi wa chuo na wanafunzi.

Watoa mada walikua ni Dokta Jafari Mussawi, Dokta Ali Swaaigh na Dokta Ridwa Sharifi, wameelezea kirusi cha Korona na historia ya kupatikana kwake pamoja na njia za maambukizi yake, na viungo vinavyo shambuliwa na maradhi hayo, kisha wakakaribisha maoni ma maswali kutoka kwa washiriki.

Kiongozi wa idara ya mafunzo endelevu katika chuo cha udaktari Hasanaini Shubbir ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Baada ya kusambaa kirusi hicho nchini China na nchi zingine zikiwemo nchi jirani, imekua lazima kufanya juhudi za kujikinga na kirusi hicho, jambo hilo ndio limesababisha chuo kikuu cha Alkafeel kuandaa darasa mjadala, ambalo tunahimiza kufuata maelekezo ya wataalamu wa afwa na kuacha kuyapuuza, kuchukua hatua za kujilinda mapema kabla maradhi hayajaingia, kutokana na kutokuwepo kwa dawa ya maradhi hayo kwa sasa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: