Kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeshiriki maonyesho ya vitabu katika chuo kikuu cha Basra yanayo fanywa kwa mwaka wa pili, chini ya usimamizi wa maktaba kuu ya chuo.
Maonyesho yamepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wakufunzi na wanachuo pamoja na watafiti wa mambo ya Basra.
Watu waliotembelea maonyesho hayo wamefurahishwa na machapisho ya kituo, kwani yamejaa turathi nyingi, wakasema kua machapisho hayo yanaonyesha historia kwa ndani.
Ushiriki huu ni sehemu ya ratiba maalum ya kushiriki katika shughuli tofauti za kijamii, na kuendeleza mahusiano mema kati ya kituo na taasisi za elimu ya sekula, banda la kituo lina aina tofauti za machapisho ya vitabu na majarida ya turathi za Basra pamoja na nakala kale adimu za Basra.