Wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika mji wa Karkuki wanatoa elimu ya kujilinda na virusi vya Korona.

Maoni katika picha
Wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) katika mkoa wa Karkuki wanatoa maelekezo ya kujilinda na virusi vya Korona, kazi hiyo ni miongoni mwa kazi za kibinaadamu zinazo fanywa na kikosi hicho.

Kuhusu shughuli hiyo tumeongea na msemaji wa kikosi, amesema kua “Kazi hii imehusisha ugawaji wa vifaa vya kujikinga bure kwa wananchi, pamoja na kugawa vipeperushi vinavyo onyesha namna ya kujilinda na virusi hivyo, sambamba na kuwajengea uwelewa na kuwahimiza wawahi kwenda kituo cha afya mara tu watakapo ana dalili za maradhi hayo”.

Akasisitiza kua: “Kazi hii ni sehemu ndogo ya kuwatumikia ndugu zetu wakazi wa Karkuki, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awalinde na awape afya nyema pamoja na raia wote wa Iraq”.

Tambua kua Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinaendelea kutoa huduma za kibinaadamu katika sekta tofauti na mikoa tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: