Maahadi ya Quráni imefanya warsha kuhusu namna ya kujikinga na virusi vya Korona

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya warsha katika mji wa Karbala, na kuhudhuriwa na jopo la wahudumu wa Maahadi pamoja na vikundi tofauti vya watoa huduma vilivyo enea kila sehemu ya Iraq.

Jambo hilo ni sehemu ya kutekeleza maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, ambaye amesisitiza umuhimu wa kuchukua tahadhari ya kusambaa kwa ugonjwa wa Korona, imejadiliwa namna ya kujikinga na kuchukua tahadhari, warsha hiyo imesimamiwa na mkuu wa Maahadi ya Quráni Shekh Jawadi Nasrawi, ambae amesisitiza ulazima wa kufuata maelekezo na kuyafanyia kazi, amehimiza watu juu ya ulazima wa kujilinda, kwani ndio njia muhimu ya kuondoa hatari hiyo.

Nasrawi akasisitiza ulazima wa kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na wizara ya afya ya Iraq na idara ya tiba katika Atabatu Abbasiyya, ya kudumisha usafi na kuvaa maski (vifaa maalum vya kuzuwia maambukizi) pamoja na njia zingine za kujikinga.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya kupitia vitengo vyake tofauti, imechukua tahadhari kadhaa za kuwalinda wafanyakazi wake na mazuwaru watukufu kutokana na maambukizi ya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: