Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) anasema: Rajabu ni mwezi wa kuomba msamaha umma wangu, ombeni msamaha kwa wingi hakika yeye ni mwingi wa kusamehe, mwezi wa Rajabu umeitwa Aswabu kwa sababu humwagwa rehme kwa wingi katika umma wangu, semeni kwa wingi kauli isemayo: (Astaghfirullaha wa as-aluhu tauba).
Kuna nyeradi nyingi ambazo zinapendekekezwa kusomwa na waumini wamehimizwa wazisome, miongoni mwake ni katika usiku wa Ijumaa ya kwanza huitwa Raghaaib, ambao ni usiku wa Ijumaa ya kwanza katika kila mwaka.
Maana ya usiku wa Raghaaibu ni usiku wa kutoa sana, usiku huo unaheshima kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, huongezeka malipo na thawabu kwa atakaefunga mchana na akaswali usiku wake na kusoma dua pamoja na kufanya mambo mema, katika husiku huo wale waliofunga na kuomba msamaha hukidhiwa haja zao na kupewa wanavyo vitaka, ndio maana malaika wakauita “Usiku wa Raghaaib).
Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) anasema: (… Msighurike na usiku wa Ijumaa ya kwanza –katika mwezi wa Rajabu- hakika usiku huo unaitwa na malaika kua Usiku wa Raghaaib, inapo fika theluthi ya usiku huo malaika wote wa mbinguni na ardhini hukusanyika katika Kaaba na maeneo yanayo izunguka, na Mwenyezi Mungu huwaambia: Enyi malaika wangu niombeni mnacho taka? Halafu wao husema: Ewe Mola wetu tunakuomba uwasamehe waliofunga Rajabu. Mwenyezi Mungu huwaambia, nimesha wasamehe).
Ni vyema kwa muumini anayetaka utukufu autumie usiku huu kumuomba Mwenyezi Mungu amsamehe dhambi zake na amridhie na kumuwafikisha kila jambo la kheri hakika yeye ni mwingi wa kusikia na mwingi wa kujibu na kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu.