Maoni katika picha
Mkuu wa kiwanda cha visafishio bwana Salaam Suleiman ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tumeongeza kiwango cha uzalishaji wa bidhaa zinazo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud, kutokana na ukubwa wa mahitaji ya idara za afya na watumiaji kutoka mikoa yote ya Iraq”.
Akaongeza kua: “Watumishi wameanza kufanya kazi kwa zamu tatu kila siku, saa zote kwa ajili ya kuziba pengo la upungufu uliopo na kukidhi mahitai”.
Akaendelea kusema: “Tunasisitiza kua bei za bidhaa zetu hazija panda wala kubadilika kwenye soko la Iraq, kwa sababu sisi wakati wote husimama pamoja na watumiaji, hasa katika mazingira magumu kama haya ambayo taifa letu linapitia kwa sasa”
Mkuu wa idara ya afya katika hospitali ya Husseini Dokta Anuwar Swadiq Dahaan amesema: “Tunashukuru juhudi zinazofanywa na shirika la Khairul-Juud, kwa kuongeza kiwango za uzalishaji wa bidhaa za usafi na kinga (maski) na kuzisambaza kwenye hospitali na vituo vya afya bila kupumzika, sambamba na kuongeza kiwango cha uzalishaji na kudhibiti mfumko wa bei”.