Madaktari wa Atabatu Abbasiyya wanafuatilia kwa karibu utekelezaji wa kujilinda na virusi vya Korona

Maoni katika picha
Kiongozi wa idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Usama Abdulhasan Kaadhim amesema kua madaktari wa idara yake wanafuatilia kwa karibu utekelezaji wa njia za kujilinda na virusi vya Korona, utekelezaji huo unaofanywa na vitengo vyote vya Ataba tukufu.

Akaongeza kua: “Vitengo vyote vimepewa visafishio na maski zinazo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud, kwa ajili ya kutumiwa kama ilivyo pangwa”.

Akabainisha kua: “Kazi ya kugawa maski kwa mazuwaru inaendelea katika milango yote ya Ataba, sambamba na kufanyia usafi mazulia na kuyawekea kinga pamoja na kuyaweka kwenye mifuko maalum, katika kitengo cha mgahawa vimewekwa vyombo vya kutumiwa mara moja tu”.

Akasisitiza kua: Tumetumia teknolojia ya Maikrojen katika kulinda eneo la ndani ya haram, hiyo ndio njia bora zaidi na imesajiliwa na wizara ya afya ya Iraq na katika (ISO), (CE), (EPA), (FDA) njia hiyo imefanikiwa kwenye nchi tofauti.

Akasema: “Tumekwenda katika mikoa tofauti kuwaeleza wananchi kuhusu namna ya kujilinda na maradhi hayo pamoja na kugawa vipeperushi”.

Tambua kua idara tajwa iliandaa warsha kubwa ya kuelezea maradhi ya Korona na namna ya kujilinda nayo pamoja na maradhi mengine ya kuambukiza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: