Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya zinaomboleza kifo cha Imamu Haadi (a.s).

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri siku ya Ijumaa mwezi (3 Rajabu 1441h) sawa na (28 Februari 2020m) maukibu ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya imeomboleza kifo cha Imamu wa kumi Ali bun Muhammad Haadi (a.s) na kumpa pole Hujjat Muntadhar (a.f) na bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maukibu (matembezi) yalianzia ndani ya haram tukufu ya Abbasi, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) walisimama kwa mistari huku wakiimba kaswida za huzuni zinazo ashiria ukubwa wa msiba uliotokea katika nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Baada ya hapo wakaelekea katika malalo ya bwana wa watu huru, wakipita katika uwanja wa kazikati ya haram mbili huku wakipiga vifua vyao (matam) na kusema mameno yanayotia huzuni kubwa kutokana na kifo cha Imamu Haadi (a.s).

Walipo wasili katika haram ya Imamu Hussein (a.s) wakapokelewa na ndugu zao wanaofanya kazi katika Atabatu Husseiniyya tukufu, wakafanya majlisi ya kuomboleza kwa pamoja ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) huku kundi kubwa la mazuwaru wakishiriki kwenye majlisi hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: