Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu: Ni wajibu kuamiliana na virusi vya (Korona) kwa tahadhari sio kwa vitisho na khofu.

Maoni katika picha
Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai amehimiza ulazima wa kufuata maelekezo ya kidaktari katika kujikinga na virusi vya Korona wala sio kutumia vitisho na khofu.

Ameyasema hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya haram tukufu ya Imamu Hussein leo mwezi (3 Rajabu 1441h) sawa na (28 Februari 2020m).

Akaongeza kua: “Vyombo vya habari vinaonyesha namna ugonywa huo unavyo sambaa kwa kasi hadi katika nchi zilizo endelea zenye uwezo mkubwa wa kidaktari na mambo ya afya, pamoja na nchi jirani, jambo hili linaashiria ulazima wa kuwa na tahadhari zaidi hususan katika maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu”.

Akabainisha kua: Inapasa kuendelea kujenga uwelewa kwa kutumia njia tofauti za mawasiliano, pia kila mtu anatakiwa achukue tahadhari ya kujilinda.

Akasisitiza kua: Inatakiwa kutoamini baadhi ya mambo yanayo tangazwa kua yana athari bila uthibitisho wowote kutoka sekta za afya zenye kuaminika.

Akasema: Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu hadi sasa bado maradhi hayo hayajaingia katika taifa letu, jambo linalo tusukuma kuendelea kuchukua tahadhari zaidi, haifai kutishana na kutiana khofu katika swala hili, kwani kufanya hivyo kunaweza kupunguza umakini wa kujilinda na maradhi hayo.

Akaonyesha ulazima wakushirikiana watu wote katika familia, shuleni, chuoni na kila mahala kwa ajili ya kuunganisha nguvu ya kupambana na hatari ya kuingia maradhi hayo hapa nchini.

Akahimiza kufuata maelekezo yanayo tolewa na idara ya afya, na kuchukua tahadhari zote za kiafya kwa ajili ya kujilinda na maradhi hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: