Nukta muhimu zilizo katika khutuba ya Ijumaa

Maoni katika picha
Khutuba ya pili katika swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein leo (3 Rajabu 1441h) sawa na (28 Februari 2020m) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai, amezungumza nukta nyingi zinazo endana na mazingira halisi tunayo ishi kwa sasa, kubwa ikiwa ni namna ya kujilinda sisi wenyewe na familia zetu pamoja na jamii kutokana na hatari ya virusi vya Korona, zifuatazo ni nukta muhimu kuhusu swala hilo:

  • - Tunasisitiza umuhimu wa uwelewa wa kiafya na kufuata maelekezo ya kidaktari katika maswala ya afya ya mwanaadamu.
  • - Afya njema ni nguzo muhimu katika maisha ya mtu na jamii.
  • - Nguvu ya jamii katika kufanya mambo tofauti kwenye maisha na kutafuta maendeleo na mafanikio, inategemea afya njema na kufuata maelekezo ya kidaktari kwa wanajamii.
  • - Mafuhumu sahihi ya afya ni pale mwanaadamu atakapokua na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kimwili, kinafsi na kiakili kwa kutekeleza majukumu ya lazima kwake na kwa jamii.
  • - Miongoni mwa misingi ya kuongeza uwelewa wa mambo ya afya, ni kufuata maelekezo ya wataalam wa afya wala sio kutoka kwa wasiokua na elimu ya afya, jambo hili ni muhimu katika maisha.
  • - Lazima tujue kua mambo ya afya ni lazima yazingatiwe na kila mtu katika maisha, jambo hili sio la kupuuzwa, linatakiwa wafundishwe watoto na wakubwa, wahisi kua jambo hilo ni muhimu katika maisha.
  • - Lazima itolewe elimu kuhusu mambo ya afya kuanzia ngazi ya familia, shule, chuo na sehemu zote za mikusanyiko ya watu.
  • - Haitoshi kutoa elimu ya afya peke yake, ni lazima kubadilisha mfumo wa maisha ya kila siku, na mfumo wa chakula na mazingira.
  • - Mazingira yetu yanamapungufu mengi.
  • - Mazingira machafu ni miongoni mwa sababu za kupatikana maradhi ya kuambukiza.
  • - Sababu za matokeo mabaya ni kutokua na uwelewa wa kiafya au kutofuata maelekezo ya kidaktari.
  • - Ulazima wa kufuata maelekezo ya kidaktari katika kuamiliana na maradhi ya (Korona) bila kutishana wala kutiana hofu.
  • - Yapasa kuchukua tahadhari zaidi ya kujilinda kwa kufuata maelekezo yanayo tolewa na vituo vya afya.
  • - Kuzidisha utowaji wa mafunzo ya afya kwa kupitia vyombo tofauti vya habari ikiwemo mitandao ya mawasiliano ya kijamii.
  • - Kila mwananchi anatakiwa kulipa umuhimu mkubwa swala hili wala haifai kulipuuza.
  • - Inafaa kutosikiliza mambo yanayo tangazwa na watu wasiojulikana, wala hayakubaliani na sekta rasmi za afya kua yanasaidia kujilinda na virusi hivyo.
  • - Haifai kutishika na kujenga hofu kubwa juu ya maradhi hayo kwa kiasi ambacho unaweza ukapoteza umakini wa kujilinda.
  • - Inatakiwa wananchi wote tushirikiane kupambana ili virusi hivyo visiingie hapa nchini.
  • - Ni lazima kufuata maelekezo yanayo tolewa na idara za afya.
  • - Haifai kughafirika kumuelekea Mwenyezi Mungu mtukufu na kumuomba atulinde na maradhi haya pamoja na binaadamu wote, hakika maradhi haya ni alama ya wazi inayo onyesha ukuu wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: