Mtandao wa kielimu wa Marjaa: Upo katika nafasi ya juu miongoni mitandao ya kimataifa (alexa)

Maoni katika picha
Mtandao wa kielimu wa Marjaa http://almerja.com ulio chini ya mtandao wa kimataifa Alkafeel umepata nafasi ya juu katika mpangilio wa mitandao ya kimataifa (alexa), umepata nafasi ya (206) kitaifa katika mitandao yenye kuangaliwa na watu wengi zaidi hapa Iraq, na umepata nafasi ya (50,417) kimataifa.

Unaweza kuingia katika mtandao huo kwa kutumia link ifuatayo: https://www.alexa.com/siteinfo/almerja.com

Mtandao wa kielimu wa Marjaa umesanifiwa kitaalam na kisasa, unamuwezesha msomaji kupata kitu anacho tafuta kwa urahisi, umejaa elimu mbalimbali kama vile elimu ya Aqida, Fiqhi pamoja na elimu za fizikia, hesabu, sheria, uongozi, uchumi.. kuna mlango wa habari na tamaduni za kiislamu sambamba na habari muhimu za afya na teknolojia pia kuna mlango unaoitwa (kalam zenye rangi tofauti).

Kutokana na jinsi mtandao huo ulivyo sanifiwa asilimia kubwa ya wanufaika wake wanatoka Iraq na nchi za kiislamu, asilimia kubwa ya wanao ingia kwenye mtandao huo wanatumia google ya kimataifa na google ya Iraq, pamoja na app zingine za kutafuta.

Kumbuka kua mtandao wa (www.alexa.com) ni mtandao wa kimataifa uliosanifiwa kisasa, makao yake makuu yapo nchini Marekani, unaendana na kiwango cha waingiaji wa mtandaoni pamoja na watu wanaofungua mitandao ya kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: