Zaidi ya ziara (9000) zimefanywa kwa niaba na mtandao wa kimataifa Alkafeel.

Maoni katika picha
Mtandao wa kimataifa Alkafeel, mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu –umefanya ziara, swala na dua- maalum katika ziara ya Imamu Baaqir na mjukuu wake Imamu Haadi (a.s) kwa niaba ya watu waliojiandikisha kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba wenye lugha za (Kiarabu, Kiengereza, Kifarsi, Kituriki, Kiurdu, Kifaransa, Kiswahili, Kijerumani) jumla ya watu waliofanyiwa ziara kwa niaba ni zaidi ya (9000) kutoka nchi tofauti.

Kwa mujibu wa watekelezaji wa huduma hiyo, ambayo mtandao wa Alkafeel ulikua mstari wa mbele, wamefanyiwa ibada hizo katika malalo takatifu, ziara ya Imamu Baaqir (a.s) imefanywa katika kaburi lake tukufu huko Baqii Ghardaq katika mji wa Madina, na ziara ya Imamu Haadi (a.s) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake na kufa kwake imefanywa kwenye kaburi lake takatifu huko Samaraa.

Usajili wa ziara hii ulidumu kwa muda wa siku tano, ili kutoa fursa ya kujisajili idadi kubwa, asilimia kubwa ya waliojisajili wametoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Iran, Lebanon, Pakistan, Urusi, Marekani, Uingereza, India, Saudia, Swiden, Kanada, Kuwait, Malezia, Australia, Aljeria, Baharain, Misri, Ujerumani, Islandi, Namsa, Yunani, Holandi, Tunisia, Denmak, Norwei, Qatar, Ubelgiji, Moroko, Afghanistan, Oman, Ekuwado, Brazili, Ajentina, Uswisi, Naijeria, Gana, Yemen, Indonesia, Italia, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Adharbaijan, Qabrus, Tailand, China, Ailand, Japani, Imaraat, Sudani).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: