Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya miongoni mwa ratiba yake ni kutoa mihadhara elekezi kila siku kalibu na wakati wa Dhuhurain au nyakazi zingine, mihadhara hiyo hua mingi zaidi wakati wa ziara maalum au miezi maalum kama vile mwezi wa Rajabu, Shabani na Ramadhani, pamoja na wakati wa maombolezo ya Ashura na Arubaini.
Mihadhara ni sehemu ya ratiba ambayo huandaliwa na kitengo hicho na hutekelezwa na masayyid pamoja na mashekh wanaofanya kazi kwenye kitengo hicho, huongelea vipengele mbalimbali kutokana na tukio husika, mada hua na maudhui elekezi katika somo la Fiqhi, Aqida, Akhlaq pamoja na hukumu za Ibada.
Rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya Shekh Swalahu Karbalai amesema kua: “Mihadhara inatolewa kila siku karibu na wakati wa Dhuhurain, mhadhiri hua ni mmoja wa mashekh wanaofanya kazi kwenye kitengo cha Dini mwenye uwezo mzuri kielimu wa kutoa mihadhara na kujibu maswali ya mazuwaru, kila swali hujibiwa kwa wazi ili wengine wapate faida, mihadhara hiyo ni endelevu mwaka mzima”.
Kumbuka kua kutoa mafundisho ya Dini ni miongoni mwa kazi muhimu zinazo fanywa na kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, na inaratiba maalum ya kutoa mihadhara na kujibu maswali ya mazuwaru.