Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huu, ikiwa ni pamoja na kufanya majlisi ya wanawake kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Imamu Haadi (a.s), majlisi hiyo imefanywa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwenye sardabu ya Imamu Jawaad (a.s), imehudhuriwa na mazuwaru wengi pamoja na wakina mama wa Zainabiyyaat wanaofanya kazi katika Ataba tukufu.
Bibi Taghrida Tamimi ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu maombolezo hayo, amesema kua: “Majlisi ni sehemu ya harakati za kuomboleza zilizo ratibiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuhuisha msiba huo, kulikua na muhadhara pamoja na igizo, muhadhara ulihusu utukufu wa Imamu Haadi (a.s) na nafasi yake tukufu aliyopewa na Mwenyezi Mungu, pia akaongelea historia ya safari ya maisha yake ya miaka arubaini, miaka ambayo walimwengu walinufaika nae sana pamoja na kubanywa na watawala wa zama zake, ilikua miaka mifupi lakini yenye faida kubwa”.
Akaongeza kua: “Kulikua na vipengele vingine vya uombolezaji, ziliimbwa tenzi na mashairi kuhusu msiba huo, mwisho wa majlisi hiyo wahudhuriaji wote walinyanyua mikono na kumuomba Mwenyezi Mungu alete faraja ya Imamu wa zama (a.f) na awanusuru wairaq na nchi zote za kiislamu”.